Yule kiungo
aliyekuja kufanya majaribio Azam FC, Ryan Burge raia wa Uingereza, kesho
Jumanne anatarajiwa kurejea kwao baada ya kushindwa majaribio.
Iwapo
kiungo huyo angefuzu katika majaribio yake, angekuwa raia wa pili wa Uingereza
kucheza Ligi Kuu Bara baada ya Kally Ongala aliyewahi kucheza Yanga na Azam FC.
Azam ilionekana
kuwa katika hatua za kumsajili Burge lakini ikafuta mpango huo na nafasi yake
ikachukuliwa na straika Mkenya, Allan Wanga aliyesajiliwa kutoka El Merreikh ya
Sudan.
Burge,
alisema anaondoka kesho Jumanne kurejea England ambako amesema kuna timu
inayomuhitaji hivyo atajiunga atakapofika.
“Natarajia
kuondoka Jumanne (kesho) kurejea nyumbani kwa sababu mambo yangu hayakuweza
kufanikiwa hapa, lakini huko kuna timu imeonyesha nia ya kunitaka na tayari tumefanya
mazungumzo ya awali.
“Sijakata
tamaa na soka la Tanzania kwani nimepanga kurejea tena siku yoyote iwapo
itatokea timu nyingine ya hapa ikinihitaji kwani nimevutiwa na mazingira niliyoyakuta
Azam licha ya kushindwa kusajiliwa,” alisema Burge.
0 COMMENTS:
Post a Comment