Vyombo vya habari vya Ureno na Hispania vimetoa mpya
baada ya kuandika kuwa kipa mpya wa Porto, Iker Casillas kwamba amekutana na
adui yake Kocha Jose Mourinho.
Hata hivyo haikuwa kweli kwamba wawili hao walikutana ‘live’
baada ya Casillas kutua Porto.
Casillas alikutana na sanamu la Mourinho ambalo liko
kwenye makao makuu ya klabu hiyo katika sehemu maalum ya jumba la kumbukumbu.
Mourinho alipata mafanikio makubwa akiwa FC Porto
kabla ya kwenda England kuinoa Chelsea.
Casillas ambaye hakuwa akielewana na Mourinho
walipokuwa Real Madrid, alipokelewa na rais wa Porto, Pinto da Costa na
kutembezwa katika sehemu mbalimbali za klabu hiyo ikiwemo kwenye jumba hilo la
kumbukumbu.








0 COMMENTS:
Post a Comment