Timu ya Al Shandy kutoka nchini Sudan, Al Malakia
kutoka Sudan Kusini na KMKM kutoka Visiwani Zanzibar zinatarajiwa kuwasili
kesho jijini Dar es salaam tayari kwa ushiriki wao kwenye michuano ya kombe la
Kagame.
Al Shandy wanatarajiwa kuwasili kesho Alhamisi saa 3
kamili asubuhi kwa usafiri wa shirika la Ndega la Kenya (KQ), KMKM wakitarajiwa
kuwasili majiraa ya saa 5 kamili asubuhi kwa boti ya Kilimanjaro, na Al Malakia
wakitarajiwa kuwasili saa 10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air.
Viwanja vya mazoezi vitakavyotumika kwa timu
zinazoshiriki michuano ha Kagame ni Chuo cha Ualimu (Duce), TCC – Chang’ombe,
Sekondari ya Loyola, Bora Kijitonyama, Polisi Kurasini, Chamazi, Uwanja wa
Uhuru.
Timu 11 zitafikia katika hoteli za Durban (Mnazi
Mmoja), Chichi (Kinondoni) Ndekha, Grand Villa, Travertine (Magomeni), wakati
wenyeji Azam na Yanga watakua na kambi zao kwa ajili ya mashindano hayo.
Wasifu wa Al Khartoum:
Al Khartoum ni kati ya wawakilishi wawili wa Sudan
kwenye kombe la Kagame. Al Khartoum ni kiboko ya vigogo katika Ligi ya
Sudan kutokana na kutoa upinzani mkali katika ligi ya nchi hiyo inayozijumuisha
timu za Al Hilal, El Merreikh na Al Shandy.
Wachezaji wa kuangaliwa:
Mshambuliaji Ismail Baba ambaye ni mchezaji wa zamani
wa Coton Sports ya nchini kwao, Kameruni anategemewa kuongoza safu ya
ushambuliaji ya timu hii kutoka jiji la Khartoum.
Kiungo mshambuliaji, Dominic Aboy, raia wa Sudani
Kusini anategemewa kuonesha ufundi katikati ya dimba. Salah Al Amini ni
mchezaji mwingine wa kutupiwa jicho.
Benchi la ufundi:
Katika kujaribu kufurukuta kutoka kwenye ubabe wa timu
mbili maarufu za Sudan, Al Merriekh na Al Hilal, wawakilishi hawa wa Sudani
walivuka mipaka na kumuajiri kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ghana, Kwesi
Appiah.
Huu utakuwa mtihani wa pili mkubwa kwa kocha Kwesi
Appiah baada ya kushindwa kufurukuta kwenye mashindano ya kombe la Shirikisho
mbele ya Power Dynamos ya Zambia.
Kundi ililopo:
Al Khartoum iko kwenye kundi A la michuano ya kombe la
Kagame kwa mwaka huu ikijumuishwa pamoja na Yanga, Gor Mahia ya Kenya, KMKM ya
Zanzibar na Telecom ya Djibout.
Bila shaka ni kundi gumu kwenye michuano ya mwaka huu.
Rekodi kombe la Kagame:
Al Khartoum ni wageni wa mashindano haya. Rekodi ya
kubwa nje ya Sudan, ni kufanikiwa kufika kwenye hatua ya kumi na sita bora ya
mashindano ya Kombe la shirikisho la CAF mnamo mwaka 2011.
Wasifu wa KMKM
Klabu ya KMKM itawaiwakilisha Tanzania kwa
upande wa Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza
Jumamosi kwenye viwanja vya Taifa na ule wa Karume.
Historia ya KMKM kwenye Kombe la Kagame:
Imeshiriki mara kadhaa bila kushinda taji hili.
Ushiriki wao haukuwa mzuri kwenye michuano ya mwaka jana iliyofanyika
jijini Kigali, Rwanda.
Hata hivyo, KMKM wameonesha nia ya kufanya vizuri
mwaka huu kwa kufanya maandalizi mapema.
Tayari wamecheza mechi tatu mfululizo za kirafiki kama
sehemu ya maandalizi yao ya kujaribu kufungua ukurasa mpya wa kufanya vyema
kwenye mashindano ya Kagame.
Benchi la Ufundi:
KMKM iko chini ya kocha mzoefu Ali Bushiri.
Wachezaji wa kuangaliwa:
Kiungo mshambuliaji, Juma Bwawa, mshambuliaji Matheo
Anthony na Hamisi Ally ni miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi ya kuisadia
klabu hii. Wengine ni pamoja na mlinzi Khamisi Ally, na Musa Saidi.








0 COMMENTS:
Post a Comment