Licha ya kujishughulisha na sanaa ya Muziki wa Bongo Fleva, Hamis
Baba ‘H Baba’, ameamua kujiunga na kikosi cha Toto Afrika ya Mwanza kwa ajili
ya kukitumikia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi
kuanzia Agosti 22, mwaka huu.
H Baba anayemudu nafasi ya ufungaji, tayari ameonekana kujiunga na
kikosi hicho huku akiwa anaendelea na mazoezi chini ya kocha John Tegete,
ambapo aliongeza kuwa keshokutwa Ijumaa ndiyo anatarajia kumalizana na uongozi
wa klabu hiyo pamoja na kusaini mkataba.
H Baba amesema alitakiwa tayari kuwa mmoja wa wachezaji wa timu
hiyo lakini kuna mambo flani ambayo bado alikuwa hajayakamilisha.
“Ilikuwa niwe nimeshamalizana na uongozi wa Toto lakini kuna
baadhi ya mambo ndiyo yalikuwa hayajakaa sawa ila mpaka Ijumaa nadhani kila
kitu kitakuwa sawa.
“Licha ya kutomalizana na uongozi wa timu hiyo, tayari
nimeshajiunga na wenzangu ambapo tayari ninaendelea na mazoezi ya kujiandaa na
msimu ujao wa ligi kuu chini ya kocha John Tegete,” alisema H Baba.








0 COMMENTS:
Post a Comment