![]() |
| KIKOSI CHA STAND MSIMU ULIOPITA. |
Unaweza kusema ni jeuri ya
fedha kwani uongozi wa Stand United umefunguka kuwa kwa sasa unasubiri kwa hamu
michuano ya Kombe la Kagame ili kupata nafasi ya kuangalia wachezaji wa
kimataifa.
Hii ni baada ya siku kadhaa
klabu hiyo kuingia mkataba wa miaka
miwili na kampuni ya Acacian ambayo
inamilikiwa na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kwa kiasi cha
bilioni mbili na milioni 400.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Aman Vincent, amefunguka kuwa wanasubiri
kwa sasa michuano ya Kagame na wao kama klabu kujipanga kuangalia uwezo wa
wachezaji ambao wanawahitaji katika kikosi chao.
Kiongozi huyo alisema katika usajili wao lazima wawe makini ili
kuweza kufanya vyema, tofauti na msimu uliopita ambapo walikuwa ni wageni wa
ligi hiyo.
“Tunataka kufanya usajili ambao utatubeba msimu ujao, lakini kwa
sasa tutampa nafasi kocha na viongozi kuifanyia kazi michuano ya Kagame
kuhakikisha tunasajili wachezaji wenye uwezo,” alisema Aman.
Ikumbukwe kikosi hicho kitakuwa chini ya makocha Patrick Liewig,
Mganda, Martin Lule na mzalendo Athuman Bilali ‘Bilo’.








0 COMMENTS:
Post a Comment