July 14, 2015


Na Aidan Mlimila 
"We give him the ball and stand back and watch.People often say to me they saw Pele and Maradona play.In the future, i will be able to say I saw Messi Play". Haya ni maneno ambayo kiungo wa zamani wa Barca Thiago Alcantara alinukuliwa akiyasema kuhusu Messi akiamini kama Messi ni mchezaj wake bora wa kizazi chake. 

Ni ukweli usiopingika kwmba Messi ni moja kati ya wachezaj bora kabisa ambao nimewai kuwashuhudia ktk kizazi hiki na kuna wengine ambao wanadiriki kumweka Messi level moja na magwiji km Edson Arantes do Nascimento(Pele) na Diego Armando Maradona Franco. 

Ni ngumu kuweza kupingana nao kwa kuangalia uwezo ambao Messi ameuthibitisha mpaka sasa lkn mm kuna vitu ambavyo naviangalia nafkiri kwa kiasi kikubwa ndivyo vinavyo watofautisha Messi na kina Pele na Maradona, kwanza nafikiri wanacheza ktk dunia mbili tofauti Maradona na Pele walicheza wkt ambao mpira ulikuwa mgumu sana ukitawaliwa kwa kiasi kikubwa na nguvu(Physical game) na wachezaj wakubwa walikuwa hawalindwi na marefa.


Tofauti na sasa ambapo kina Messi wanacheza wkt ambao kwa kiasi kikubwa technolojia imechangia kuurahisha mpira na kuufanya kuwa kitu rahisi...na wachezaj wakubwa wamekuwa wakilindwa na marefa tofauti na zamani.. 

Lakini kikubwa zaidi ambacho nafikiri kina-mark utofauti kati ya messi na kina pele ni kwenye kusaidia mafanikio ya timu ya taifa.

Mara ya mwisho Messi amevaa medali ya ushindi kwa timu ya Taifa ilikuwa ni mwaka 2008 Beijing China kwenye mashindano ya Olimpiki ambayo ni mahususi kwa wachezaj U-23 tangu hapo Messi hajawahi kupata mafanikio na senior team mafanikio makubwa yamekuwa ni kufika fainali ya Kombe la Dunia 2014 na Copa America 2015 ambapo walipoteza na Chile. Mpaka sasa ameshacheza jumla ya michuano mitatu ya Kombe la Dunia kuanzia 2006, 2010 na 2014 na hajafanikiwa kuvaa medali hata moja ya ubingwa! 

Lakini Pele ukiachilia mbali mafanikio aliyoyapata akiwa na Santos na klabu nyingne. Kwa upande wa timu ya taifa ameshavaa medali 3 za world cup kati ya fainali nne alizocheza (1958,1962,1970) huku yeye akichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo. 

Pia Maradona katika fainali nne alizocheza za Kombe la Dunia ameisaidia timu ya taifa kutwaa ubingwa mwaka 1986 kule Mexico kwenye mechi fainal dhidi ya West Germany lakini pia mwaka 1990 aliiwezesha timu yake kufika fainal nchini Italia. Lakini walifungwa na West Germany mechi iliyochezwa Stadio Olimpico jijini Roma. 

Na hapa ndipo ambapo naona Messi anakimbiza vivuli vya pele na Maradona bila mafanikio, although tayari amesha prove yeye ni mchezaj wa aina gani lakini nafikiri anahitaji kufanya kitu akiwa na jezi za timu ya taifa kwanza.. 

MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA AIDAN MLIMILA AMBAYE NI MSOMAJI WA BLOGU YA SALEHJEMBE...


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic