Timu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini ‘Sauz’,
imetoa msimamo kuhusiana na majaribio ya kiungo wa Simba, Jonas Mkude
aliyekwenda nchini humo kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwa wiki
mbili.
Mkude alirejea nchini kimyakimya mara baada ya
majaribio hayo huku kukiwa hakuna kauli rasmi juu ya majaribio aliyoyafanya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,
Zacharia Hans Poppe amefunguka hivi:
“Mkude siyo kwamba ametoswa moja kwa moja kule
Wits isipokuwa wamesema walikuwa na wachezaji wengi wa majaribio, hivyo yeye
(Mkude) amerejea nchini kisha wataendelea kumfanyia tathmini ya kina katika
ligi ya nyumbani.
“Wametoa miezi mitatu ya kumchunguza kisha baada
ya hapo watakuwa na kitu cha kutuambia kama wameridhika naye au la.”
Tokea Mkude arejee kutoka Sauz kumekuwa na taarifa zinazokinzana wengine wakiamini amefeli ndiyo maana kila kitu kimekuwa kimyakimya.
Hizo siasa tu, kachemka!! Miezi mitatu watamsajili kwa msimu gani!!?
ReplyDelete