| JULIO AKIWA NA KIKOSI CHAKE CHA MWADUI BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI DARAJA LA KWANZA. |
Kocha Mkuu
wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ameendelea kutamba kuwa kikosi chake
kitakuwa hatari msimu ujao na kudai kuwa yuko makini katika kuhakikisha
anatengeneza kombinesheni ambayo itafanya vizuri hasa kwenye safu ya
ushambuliaji.
Kocha huyo
anatafuta kombinesheni ya Paul Nonga, Rashid Mandawa, Bakari Kigodeko na Kelvin
Sabato.
Julio
ambaye yupo na Mwadui kambini katika Mgodi wa Mwadui mkoani Shinyanga, amesema
timu yake haichezi michezo ya kirafiki mpaka pale atakapokamilisha kutengeneza
kombinesheni kwenye kikosi chake.
“Watu
wanaweza kusema najisifu lakini hapa ukweli wachezaji niliosajili safari hii ni
wazuri, Mwadui itakuwa tishio msimu ujao na kwa sasa katika fundisha yangu
kikubwa natengeneza kombinesheni kuhakikisha wachezaji wanakuwa vizuri, hasa
mbele kwenye safu ya ushambuliaji.
“Nikimalizana
na hilo ndiyo nitafikiria kuanza kutafuta michezo ya kirafiki maana hapo ndiyo
kikosi changu kitakuwa vizuri, kule wakikutana na Nonga inakuwa balaa,” alisema
Julio.







0 COMMENTS:
Post a Comment