Kiungo
mpya wa Azam FC, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’, amepewa jezi namba 16 ambayo
iliwahi kuvaliwa na Mrisho Ngassa alipokuwa klabuni hapo, lakini habari mbaya
ni kuwa ameng’oka jino akiwa mazoezini.
Migi, raia wa Rwanda, amejiunga na Azam FC hivi karibuni na kusaini
mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo akitokea APR ya nchini kwao.
Migi ameiambia SALEHJEMBE kuwa
hajui kama atashiriki katika michuano ya Kombe la Kagame kwa kuwa ameng’oka
jino akiwa mazoezini.
Migi alijibu hivyo baada ya kuulizwa juu ya timu atakayoichezea katika
michuano hiyo ya Kagame. “Nilitakiwa kuichezea Azam na siyo APR, lakini sijui
kama nitacheza tena kwa kuwa nimepata tatizo kwa kung’oka jino nikiwa mazoezini
leo (jana).
“Nilikuwa hospitali, jina silijui lakini ni maeneo ya Temeke,
nimeambiwa natakiwa kupumzika kwa wiki moja,” alisema Migi. Alipopigiwa Daktari
wa Azam FC, Mbarouk Mlinga, simu yake haikupokelewa.







0 COMMENTS:
Post a Comment