July 31, 2015


Na Nassor Amour, Zanzibar
Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, ambaye juzi Jumatano alikiacha kikosi chake kikiendelea na mazoezi kisiwani Zanzibar na kwenda Uwanja wa Taifa jijini Dar kushuhudia robo fainali ya Kombe la Kagame, kati ya Yanga na Azam, amesema Yanga ni timu ya kawaida sana.


Kocha huyo amesema anashangaa viongozi wake kumueleza kila siku kuwa aifunge Yanga wakati yeye anaiona ya kawaida sana.
Akizungumza mjini hapa, Kerr alisema ameiona mechi hiyo na kusema si kwamba Yanga hawana wachezaji wazuri lakini Azam walifanya vizuri zaidi licha ya kwenda sare mpaka kufikia hatua ya matuta.

 “Kutokana na msisitizo huo, nimelazimika kufuatilia baadhi ya mechi za timu hiyo, nimeona mambo kadhaa lakini sioni la ziada katika timu hiyo nikiilinganisha na kikosi changu ambacho nasikia nitaletewa wachezaji wengine wa kimataifa kwa ajili ya kukiimarisha.

“Yanga waliocheza juzi ni wa kawaida sana na hawatishi,” alisema Kerr.


Hii ni mara ya pili kocha huyo wa Simba akitamkia neon hilo kwamba Yanga ni timu ya kawaida sana.

1 COMMENTS:

  1. Makocha wote wa simba wakija wanasema yanga ni timu ya kawaida,lakini mbona hamuwanyang'anyi hizo namba nanyi mkaenda kimataifa?Hatutaki sifa za kijinga, tunataka kombe msimbazi safari hii.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic