July 10, 2015



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa kali baada ya kusema amesusia kununua vitu vinavyotengenezwa na kampuni ya Azam FC.

Hans Poppe amesema hatakuwa akinywa maji ya Azam wala kula kesi za Azam kwa madai wamewafanyia ‘uhuni”.

Hans Poppe ameyasema hayo leo wakati akihojiwa la E FM Radio kwa madai Azam FC wamefanya hila kuhakikisha wanampata kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’ kwa hila.

“Wamemsajili Messi kwa ujanja, wameshinikiza hili suala ili wampate kijanja. Nasema mimi sasa sitakula keki zao wala kunywa maji yao.
“Ndiyo, nafanya hivyo ili kupunguza nguvu. Maana kama tunanunua vitu vyao tunawapa nguvu halafu wanatudhulumu,” alisema.

Messi ametua Azam FC baada ya kamati ya maadili na hadhi za wachezaji ya TFF kuvunja mkataba wake.


Simba wamekuwa wakilaumu uvunjwaji huo wa mkataba unaonyesha kuwa wa mipango.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic