Leo Jumamosi Simba inatimiza siku sita tangu ilipoanza kambi yake
wilayani hapa kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, ila mipango yake
inatibuliwa na hali ya hewa ikiwemo baridi na mvua.
Awali, kikosi hicho kilichokuwa kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Chuo cha Magamba, jana Ijumaa kililazimika kufanyia mazoezi yake kwenye Uwanja
wa Chuo cha Irente Rainbow kutokana na barabara kuharibiwa vibaya na mvua
zinazoendelea kunyesha kila siku.
Simba haitakuwa na mchezo wowote wa kirafiki mpaka itakapohamishia
kambi yake visiwani Zanzibar.
Kocha Dylan Kerr anaonekana kuifurahia hali ya hewa ya hapa ambayo
ni ya baridi kali lakini imekuwa tofauti kwa wachezaji ambao wanalalamika kila
siku. “Ukiachana na mambo mengine kama ubovu wa barabara, mimi nimeridhika na
hali ya hewa ya hapa,” alisema Kerr.
Jana Ijumaa wachezaji wa Simba waliokuwa Taifa Stars, walitarajiwa
kujiunga na kambi ya timu hiyo ambao ni Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Said
Ndemla na Hassan Isihaka. Pia Jonas Mkude aliyekuwa Afrika Kusini naye
alitarajiwa kuwasili.
0 COMMENTS:
Post a Comment