KMKM imejiweka katika wakati mgumu kwenye michuano ya Kagame baada ya kupoteza matumaini kutokana na kupoteza mechi yake ya pili baada ya kufungwa
mabao 2-0 na Kharthoum ya Sudan.
Mechi hiyo imepigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Kupoteza huko, kunaifanya KMKM
ibakize matumaini katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Yanga.
Iwapo itashinda dhidi ya Yanga, KMKM
itakuwa imesonga mbele, lakini ikipoteza itakuwa imeyaaga mashindano.
Kwani licha ya kuanza vizuri kwa
ushindi, KMKM imepoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Gor Mahia na leo dhidi
ya Wasudan.
0 COMMENTS:
Post a Comment