Yanga imerejea katika michuano ya
Kagame baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibout katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo, Yanga ilianza kwa kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Gor Mahia huku mshambuliaji wake Donald Ngoma akilambwa kadi ya nyekundu.
Malimi Busungu ndiye shujaa baada ya
kufunga mabao mawili huku Geofrey Mwashuya, dogo kabisa akifunga bao la tatu.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa na bao moja
lililofungwa na Busungu.
Hata hivyo, Yanga ilikosa mikwaju
miwili ya penalti, akianza Amissi Tambwe ambaye mpira aliopiga ulitoka nje,
kabla ya Simon Msuva naye kupoteza penalti ya pili.
Yanga sasa itashuka tena dimbani
Ijumaa kuivaa KMKM kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment