MAKAMBA |
Na Saleh Ally
CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kiko katika harakati
za mwisho kumpata mgombea wake wa urais na leo ndiyo tatu bora inajulikana.
Tayari tano bora imeishajulikana ambayo ni Benard Membe, Asha-Rose Migiro, Januari Makamba, John Magufuri na Amina Ally.
Mgombea mmoja atatangazwa kesho na
kitendawili cha nani atakuwa mgombea wa urais wa chama hicho kikongwe nchini
kitakuwa kimetenguliwa, huenda itakuwa wakati wa kupongezana na kufutana
machozi.
Hayo tuwaachie wao wanasiasa, lakini si
vibaya kuwagusa leo kwa kuwa wenyewe waliamua kuingia katika anga zetu.
Huenda nitakaowagusa wakiwemo waliopigwa
chini kwenye tano bora, tatu bora na mwisho mgombea huyo mmoja.
Lakini nimeona si vibaya kuwakumbusha
kuhusiana na walichosema baada ya kuwa wametangaza nia ya kugombea urais
kupitia CCM.
PINDAAsilimia kubwa ya wagombea ukimtoa John Magufuli ndiyo sikuwasikia wakizungumzia masuala ya michezo. Waliobaki kwa asilimia kubwa, walizungumza, lakini mwisho waliigusa michezo. |
Nilimsikia Januari Makamba akijisifia sasa
Tanga ina timu tatu za Ligi Kuu Bara, yaani Coastal Union, Mgambo na wakongwe
African Sports ambao wamerejea.
Edward Lowassa wakati akizindua kampeni
zake, naye aliizungumzia michezo akidai akipata nafasi ya kuiwakilisha CCM,
akagombea basi michezo itapewa kipaumbele na kuna mipango lukuki.
Hali kadhalika, Benard Membe, Sospeter
Muhongo, Lazaro Nyalandu na wengine.
LOWASSA |
Kweli wapo ambao nawajua walioonyesha
angalau ushiriki wao michezoni kama Fredrick Sumaye, Samuel Sitta, Mwigulu
Nchemba lakini bado ninaweza kusema hawakuwa ‘sirias’ katika suala hilo hadi
unaweza kusema walikuwa na msaada mkubwa.
Makamu wa Rais, Dk Mohammed Ghalib Bilal na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambao wamekuwa madarakani kwa muda wote, ninaweza
kusema michezo hawakuijali kabisa kwa kubwa ni nadra kweli kusikia hata
wakizungumzia maendeleo yake.
Kwa kundi lote hili, unaposikia mmojammoja
anazungumzia michezo, hakuna ubishi nachukulia kama ni maneno ya ulaghai kwa
kuwa si watu wenye mapenzi na michezo na hawaijali.
Huenda inakuwa ni wakati mwafaka kuiingiza
katika hotuba zao wakitaka kuwakamata wanaopenda michezo kuwaona wapo pamoja
nao.
Wanajaribu kuingiza maneno matamu kuhusiana
na michezo kwa kuwa wanaijua ina nguvu kiasi gani. Hakuna ubishi hawaipendi
michezo badala yake wanapenda nguvu zake ambazo wanajua zitakuwa msaada kwao.
NYALANDUKatika wagombea hao rundo wa nafasi ya urais kupitia CCM, wengi hawana sifa ya kuizungumzia michezo na kuwathibitishia wanamichezo kwamba wana nafasi ya kuikuza na kuiendeleza. |
Lakini wakumbuke, michezo ina watu wengi
wasikivu, waelevu na wang’amuzi wa mambo, hivyo haitakuwa rahisi kuwalaghai au
kutaka kuwajaza maneno ya kijanja na kuwatumia. Halafu wakipata wanachokitaka,
wawaache kwenye mataa kama ambavyo wamekuwa wakifanya miaka yote.
Pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete anayemaliza
muda wake. Kama alivyosema katika hotuba yake ya kuvunja bunge kuwa
alijitahidi, yuko sahihi kabisa.
Wote tuliona namna alivyochangia, kweli
aliidhinisha mishahara kwa makocha wa timu za taifa za soka, ngumi, kikapu na
netiboli. Ingawa maendeleo hayakuwa makubwa sana, lakini angalau.
Bado naweza kusema Kikwete alijitahidi,
lakini serikali yake kwa kiasi kikubwa haikuwa mshiriki mzuri wa michezo na
hata watu wengi walio katika wizara husika hawapo kwa ajili ya michezo kwa kuwa
hawajasaidia lolote zaidi ya majungu kuliko utendaji bora zaidi.
Hivyo, mapema kabisa, taarifa hizi zimfikie
atakayekuwa mgombea wa CCM, yaani yule atakayejulikana kesho kwamba yeye na
wenzake, tumewasikia kuhusu michezo na akumbuke michezo ni ajira kubwa,
ikifanyiwa mipangilio bora, itatengeneza ajira nyingi zenye mishahara mikubwa
kuliko hata vitu vingine wanavyovitegemea.
Pia, kama amepata nafasi na atafanikiwa
kushinda kuwa Rais wa Tanzania, aonyeshe kweli anaipenda michezo kama kauli
walizozitoa, ana mipango nayo na si kuifanya ni sehemu ya kupita kwa ajili ya
faida yake kwa ajili ya alichotaka kukipata. Kudanganywa kwa wanaspoti,
imetosha.
0 COMMENTS:
Post a Comment