Na Saleh
Ally
WAKATI
Alex Ferguson rasmi anatua Manchester United mwaka 1986 akitokea Aberdeen ya
kwao Scotland, ndiyo Kocha Louis van Gaal alikuwa anaanza rasmi kazi ya ukocha.
Ferguson
alianza kazi ya ukocha mwaka 1974, miaka 12 baadaye, van Gaal ndiyo akaanza
kazi hiyo. Hivyo inakuwa ni rahisi kujua ubora wa makocha hawa kwa maana ya
uzoefu.
Van Gaal,
tayari ana umri wa miaka 19 katika kazi ya ukocha akifundisha nchi mbalimbali
za Ulaya kama kwao Uholanzi, Hispania, Ujerumani na sasa England akiwa Kocha
Mkuu wa Manchester United.
Amekuwa na
mafanikio makubwa akiwa na Ajax, Barcelona na Bayern Munich na zote hakuondoka
bila ya kuzipa makombe. Kazi yake inajulikana na si hadithi ngeni kuwa ni yenye
mafanikio.
Wakati
ametua Manchester United, ilionekana hakuwa na tofauti na David Moyes
aliyeshindwa kuubeba ‘mzigo’ wa klabu hiyo baada ya kuachiwa na Ferguson. Sasa
umetua mabegani kwa van Gaal na hakuna ubishi, utakwenda tu hata kwa tabutabu
hivyohivyo.
Unaweza
kushangazwa sana na namna ambavyo van Gaal amekuwa akiendelea kubaki katika
benchi kama Man United imeishachapwa bao tatu au nne. Ataendelea kubaki hapo
hata kama kuna presha kubwa. Kwa nini?
Huenda hii
ni nafasi nzuri ya kujua upande wa pili wa shilingi wa kocha huyo ambaye ana
nafasi kubwa ya kufikia kuwa mmoja wa makocha wenye uwezo huo.
Asili ya
van Gaal ni kuwa mmoja wa makocha wenye akili sana, wanaojiamini kwa
wanachokifanya na wagumu kutetereka kwa kuwa wanachoangalia cha kwanza ni
mafanikio na si fedha au kupelekwapelekwa.
Nimeanza
kusoma kitabu cha maisha ya van Gaal, ambacho baadaye kitaanza kuchapishwa
kwenye magazeti ya Championi. Mambo kadhaa niliyoyaona, nikaona ni vema
kuyaweka kwanza ili msomaji ajua kocha huyo Mholanzi ni mtu wa aina gani na
amewahi kufanya nini katika soka nje ya benchi lake la ufundi.
Bluu:
Mwaka
1977, akiwa bado mchezaji kinda tu katika klabu ya SC Telstar alizua hoja
iliyoonekana ya ajabu kabisa baada ya kuuliza uongozi wa klabu hiyo kama
inawezekana kutumia uwanja wenye muonekano wa bluu ‘blue pitch’.
Klabu hiyo
ikaona ni jambo jema kulifikisha kwa Shirikisho la Soka la Uholanzi (KNVB),
nalo likapaisha jambo hilo hadi Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ambao
walilitosa na kusema si sahihi, itawachanganya watu na jamii ya soka kwa kuwa
imezoea viwanja vya kijani ‘green pitch’, miaka nenda rudi.
Baadhi
waliposikia hilo, wakaanza kulifanyia majaribio na sasa kuna viwanja vingi vya
bluu katika viwanja vya mazoezi ya klabu kubwa ikiwa ni sehemu ya kubadilisha
hali ya hewa na kuepusha kuwachosha wachezaji na kijani.
Michezo
mingine ya soka kama futsal (ule wa ndani na uwanja mdogo unaoonekana kama wa
mpira wa kikapu), wamekuwa wakitumia viwanja vya bluu na inaonekana, chanzo ni
van Gaal, enzi hizooo.
Waamuzi
zaidi:
Van Gaal
anawekwa katika kundi la makocha ‘vipanga’, yaani wenye akili na mchango mkubwa
katika mabadiliko ya soka likiwemo jambo la kuongezeka kwa waamuzi wawili wa
pembeni katika mchezo wa soka.
Ingawa
imekuwa haizingumzwi sana, van Gaal alikuwa wa kwanza kusema kuwa waamuzi
watatu hawatoshi katika uamuzi wa soka uwanjani. Hivyo kushauri waongezwe
wengine pembeni wawili au zaidi, lakini ilionekana ni sawa na kuvuruga
utamaduni wa kisoka.
Pamoja na
kukataa wazo lake, kadiri siku zinavyosonga mbele. Wazo alililotoa, limekuwa
likiendelea kujadiliwa hadi mwisho Fifa na wadau wake lilipokata shauri kwamba
yaanze majaribio, sasa waamuzi hao wameanza kutumika hadi katika mashindano
makubwa kabisa.
Mtambo
langoni:
Baada ya
Thierry Henry kufunga bao la mkono na kuibeba Ufaransa kucheza Kombe la Dunia.
Siku chache kabla ya tukio van Gaal alikuwa ameeleza umuhimu wa kuhakikisha
kuna mitambo maalum kutambua usahihi wa bao.
Ingawa
hakuwa akizungumzia mkono au mguu uliotumika, lakini alitaka uhakika wa kuvuka
mstari au la. Jambo ambalo lilionekana ni tatizo na litaharibu ladha ya mpira.
Ingawa
hakuwa wa kwanza kulianzisha, lakini ufafanuzi wake katika makongamano kadhaa
ya Fifa na Uefa, yaliibua ushawishi upya hadi Fifa kutaka hilo lianze kufanyiwa
kazi.
Hataki
penalti:
Inawezekana
wapo wanaofikiria kama van Gaal, lakini yeye ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa
kuthubutu kila inapofikia kuna jambo amelifanyia uchunguzi na kuliona ni
sahihi.
Van Gaal
si mtu wa kujisikilizia, akitaka jambo na akaliamini basi atalisema hata mbele
ya watu ambao anajua watalikataa.
Miaka
michache kabla ya kutua Manchester United, van Gaal aliibuka na jambo jipya,
yeye akisema anapinga upigianaji penalti, anaona si sahihi na hauufanyi mchezo
wa soka kuwa “pambano la wanaume wa shoka”.
Penalti
ndani ya dakika 90, haoni tatizo, lakini ushindi wa mwisho kuamuliwa kwa ile
mikwaju mitano au zaidi anaona ni kuufanya mchezo wa soka kuwa wa watu
lainilaini.
Van Gaal,
hajawahi kupinga kitu halafu asitoke na wazo lake ambalo anaamini litakuwa
suluhisho.
Katika
hili la penalti, amesema baada ya kuongezwa dakika 90 kwisha bila kupata
mshindi. Basi zile dakika 30 zitakapoongezwa, kila baada ya dakika 5, kila timu
itatoa mchezaji mmoja nje.
Maana
yake, baada ya dakika 30, kila timu itakuwa imepoteza wachezaji sita, yaani 12
watakuwa wametoka uwanjani.
Hiyo
itaufanya uwanja kuwa mkubwa sana kwa wale wanaobaki na inakuwa rahisi timu
yoyote kufungwa kwa wakati wowote.
Mwisho
akasisitiza, mpira una maajabu na kama ikitokea dakika 120 bado bao
halijapatikana. Basi bao la dhahabu kwa muda kadhaa, ndiyo litumike kuamua.
Hili bado Fifa, Uefa na wengine hawajalifanyia kazi.
Kasi:
Katika
mkutano wa mmoja na Fifa, pia alipendekeza kuwa na mipira ya kisasa ambayo
itakuwa ikipima kasi ya mchezo ili kujua miaka ya nyuma, kasi ilikuwa kiasi
gani na kama inapanda, basi kwa kiasi gani ndani ya miaka mingapi.
Tayari
kuna makampuni yanayofanya kazi hiyo, yameishaanza kulifanyia kazi hilo lakini
baadhi ya makampuni ya vifaa vya michezo, yamekuwa yakiweka vifaa maalum kwenye
viatu vya wachezaji, kupima kasi.
Van Gaal
ana mengi kuonyesha ni kocha wa aina yake. Huenda utafurahia zaidi kufuatilia
historia ya maisha yake katika magazeti ya Championi.
0 COMMENTS:
Post a Comment