July 6, 2015


Simba imechukua uamuzi wa kumuuza Emmanuel Okwi nchini Denmark.

Okwi anakwenda kucheza soka katika kikosi cha 
Sonderjyske inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Rais huyo wa Uganda anatarajia kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Denmark kuanza kazi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kila kitu kimekamilika kuhusiana na Okwi.
“Kweli Okwi anakwenda Denmark, hii ilikuwa ni sehemu ya makubaliano kati yetu na yeye.

“Kwamba kama atapata timu nje, basi tumuachie aende.
“Wale jamaa pia wakatoa ofa nzuri, hivyo hatukuwa na ujanja zaidi ya kumuachia aende zake,” alisema Hans Poppe, hata hivyo alikataa kuweka wazi kiasi cha fedha ambacho wamemuuza.


“Hiyo inabaki kuwa siri ya Simba, maana tukitaja basi hesabu zinakuwa nyingi sana.”

1 COMMENTS:

  1. Hapo ubabaishaji ndo unapoanzia na wizi!! Mbona ulaya kila kitu kinakuwa wazi kwanini bondo ada ni siri!?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic