Kocha Mkuu wa Mwadui FC ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’,
amefunguka kuwa kwa kikosi alichonacho hivi sasa lazima timu za Simba na Yanga
zikae pindi watakapokutana kwenye mechi za ligi kuu.
Mwadui ni miongoni mwa timu nne zilizopanda daraja msimu uliopita,
zikiwemo Toto African ya jijini Mwanza, Majimaji ya Songea na African Sports ya
Tanga.
Julio tayari ameshanasa mastaa kibao wakiwemo Paul Nonga kutoka
Mbeya City, Rashid Mandawa kutoka Kagera, David Luhende kutoka Mtibwa, Shaban
Kado kutoka Coastal na Jabir Aziz aliyekuwa JKT Ruvu. Lakini imemuongezea
mkataba mkongwe Athuman Idd ‘Chuji’.
Julio amesema kuwa tayari ameshamaliza usajili kwa kupata kikosi
bora kitakachokuwa na ushindani msimu ujao na akasisitiza kuwa lazima timu za
Simba, Yanga na Azam zikae pindi watakapokutana nazo.
“Kikosi nilichokisajili ni cha kiushindani wa hali ya juu, lazima
timu kubwa za Simba na Yanga zikae pindi tutakapokutana, nashukuru Mungu kuwa
ndiyo timu pekee iliyomaliza usajili hadi sasa. Kila mchezaji wangu anaonyesha
nia ya kufanya vyema, hivyo natarajia kutoa ushindani wa kutosha msimu ujao,”
alisema Julio.
kwenada zako kwani team ni hizo tu 3 pyeeeeee
ReplyDelete