Akiwa anaichezea
Platinum FC ya Zimbabwe, Donald Ngoma aliifungia timu yake mabao 16 msimu
uliopita, lakini hivi sasa akiwa na Yanga amepanga kuongeza kasi ili afunge
mabao mengi kuzidi aliyoyapachika akiwa na klabu yake ya zamani.
Ngoma ametua
kuichezea timu hiyo hivi karibuni pamoja na Mghana, Joseph Zuttah, kila mmoja
akisaini mkataba wa miaka miwili na tayari ameshaifungia Yanga bao moja kwenye
mchezo wake wa kwanza klabuni hapo, wa kujipima nguvu dhidi ya KMKM.
Ngoma, raia wa
Zimbabwe, amesema anataka kufunga mabao mengi zaidi iwezekanavyo lakini akaomba
apewe muda ili azoeane vyema na wenzake.
“Malengo yangu ni kupita idadi ya mabao 16
niliyofunga nikiwa na Platinum kwa kuanzia mechi za ligi kuu na michuano ya
kimataifa.
“Ninaamini
nitaifikisha na kuipita idadi hiyo ya mabao niliyofunga nikiwa na Platinum na
hilo nitafanikiwa kama nitapata ushirikiano mzuri wa wachezaji wangu katika
kunipa pasi nzuri,” alisema Ngoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment