Nahodha wa Simba, Mussa Hassan Mgosi,
amewatoa hofu Yanga kwa kuwaambia wasife moyo kutokana na kuanza vibaya kwenye
michuano ya Kagame.
Yanga ilianza kwa kuchapwa mabao 2-1 na Gor Mahia
kwenye mchezo wa kwanza wa Kombe la Kagame, lakini mshambuliaji huyo wa zamani
wa Taifa Stars amewaambia wasijali, hayo ni matokeo ya kawaida.
Mgosi alisema katika soka kufungwa ni jambo
la kawaida kabisa, ambapo aliwashauri Yanga kuangalia ni wapi walikosea katika
mchezo uliopita ili kufanya vizuri kwenye michezo ijayo.
“Unajua katika soka kuna matokeo mengi, kama
hivyo, kufunga, kufungwa au sare, hivyo sioni kama Yanga walifanya vibaya sana.
“Kitu ninachoweza kuwashauri ni kuangalia
wapi walikosea kwenye mchezo dhidi ya Gor Mahia na kurekebisha ili waweze
kufanya vizuri kwenye michezo ijayo.
“Mimi binafsi ile mechi sikuiangalia, si unajua
tulikuwa kambi kwa muda mrefu na siku ile ndiyo tulirudi, hivyo sikuweza kucheki
ila kwa jinsi nilivyohadithiwa, ninaamini Yanga bado wana nafasi kubwa sana ya kufanya
mabadiliko na kila kitu kikaenda sawa na ikiwezekana wakatwaa ubingwa,” alisema
Mgosi.







0 COMMENTS:
Post a Comment