July 29, 2015


Wakati straika wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, akitarajiwa kutua kambini visiwani hapa ndani ya siku mbili hizi, mashabiki wa klabu hiyo juzi walijitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Amaan kuhudhuria mazoezi ya kikosi hicho wakiamini Mrundi huyo angekuwepo uwanjani hapo.


Lakini Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, amethibitosha kuwa, Mavugo atatua Zanzibar ndani ya siku mbili.

Matola amesema mbali na Mavugo, Simba pia inawasubiri wachezaji wengine wawili, kiungo mshambuliaji Mrundi aliyemtaja kwamba ni hatari uwanjani aliyemkumbuka kwa jina moja la Pekie na kiungo Mwinyi Kazimoto. Mashine hizo zinasubiriwa kwenda kukamilisha kikosi kazi cha Simba msimu ujao wa ligi kuu.

Pekie anatokea Vital’O kama ilivyo kwa Mavugo wakati Kazimoto ameshasaini mkataba wa miaka miwili akitokea Al Markhiya ya Qatar.


“Mwinyi atatua muda wowote kuanzia sasa, lakini Mavugo tutampokea ndani ya siku mbili hizi, atatua pamoja na kiungo mmoja mshambuliaji anayetoka naye timu moja, namkumbuka kwa jina moja la Petie,” alisema Matola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic