Taifa Stars imepangwa kucheza na Malawi
katika kufuzu Kombe la Dunia 2018 na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema
hiyo si mechi nyepesi hata kidogo na itahitajika nguvu ya ziada kuvuka
kizingiti hicho.
Mchezo wa kwanza wa timu hizo
utafanyika Oktoba 5 kisha marudiano Oktoba 13, mwaka huu na mshindi atacheza na
Algeria katika hatua inayofuata.
Cannavaro amesema wana kibarua kizito katika mchezo huo kwani anaijua Malawi
jinsi ilivyo na wachezaji makini na isionekane kama timu rahisi.
“Mechi ya Malawi si nyepesi tena, wale
jamaa wapo vizuri si wa kuwachukulia wepesi, lakini hata kama tutapita hapo,
bado kuna kazi nzito sana kwa Algeria,” alisema Cannavaro.
“Lakini tutapambana ingawa kwa sasa
hizo mechi sijaziweka sana kichwani mpaka tutakapomaliza hii michuano ya Kombe
la Kagame,” aliongeza Cannavaro ambaye pia ni nahodha wa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment