Straika mkongwe wa Simba, Mussa Mgosi,
ametamka kuwa kama timu yake inataka mabao, basi apangwe na Mganda, Hamis Kiiza
kikosini.
Washambuliaji hao wote walijiunga
kwenye kikosi cha Muingereza, Dylan Kerr hivi karibuni kwa mkataba wa miaka
miwili kuichezea timu hiyo iliyoweka kambi yake visiwani Zanzibar.
Mgosi aliyetokea Mtibwa Sugar baada ya
kumaliza mkataba wake pamoja na Kiiza, wote waliifungia Simba bao moja kila
mmoja na kuiwezesha kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kombaini ya Zanzibar
juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mgosi
amesema: “Nimemuona Kiiza akicheza mechi ya kwanza na nimekubali uwezo wake,
kama Simba inataka mabao mimi nipangwe namba tisa na Kiiza namba kumi, lazima
tufunge.”
Hata hivyo, katika mchezo dhidi ya
Kombaini ya Zanzibar, Mgosi hakufanikiwa kucheza pamoja na Kiiza kwani Kocha wa
Simba, Dylan Kerr aliwapanga katika vikosi viwili tofauti.
“Nataka kucheza na Kiiza kutokana na uwezo
wake mkubwa alionao ndani ya uwanja, isitoshe ana uzoefu mkubwa na anaweza
kutengeneza nafasi za kufunga mabao,” alisema Mgosi.
0 COMMENTS:
Post a Comment