Mashabiki wa Real
Madrid wameuangushia lawama uongozi wa klabu hiyo kwamba unapenda fedha kuliko
kuangalia maandalizi ya kikosi chao.
Wakati wapinzani wao
Barcelona wakiwa Marekani kwenye joto, wao wamejichimbia Australia ambako kuna
baridi. Mashabiki hao wamekuwa wakipinga kupitia mitandao ya kijamii, pia tovuti ya klabu hiyo.
Hali ya hewa ya
Australia sasa ni nyuzi joto 5 hadi 10, jambo ambalo wanaona si sahihi kwa
maadalizi ya timu.
Kwa hapa nyumbani,
Simba nayo ilijichimbia mjini Lushoto kwa ajili ya maandalizi ambako hali yake
ya hewa ni kama Australia.
Lakini kocha wa viungo
na mtaalamu wa chakula wa Real Madrid, Miguel Ángel Duque Cano, ameliambia
gazeti la MARCA kwamba hakuna tatizo kwa wao kufanya hivyo.
“Kwenye baridi kuna
mambo mengi, kikubwa kabla ya mazoezi wachezaji wapashe vizuri. Lakini kwenye
baridi wachezaji wanapumzika sana na hili ni jambo jema.
“Pia kufanya mazoezi
kwenye baridi kunachangia misuli kujijenga vizuri, hivyo ni sahihi kabisa,”
alisema.
Mashabiki hao walikuwa
wanaamini Madrid imekwenda kwenye baridi lakini inachoangalia ni kujitangaza
kwenye soko la Australia tu.









0 COMMENTS:
Post a Comment