| KATWILA (MWENYE FULANA YA NJANO) AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WALIOJITOKEZA KUWANIA KUSAJILIWA NA MTIBWA SUGAR....Mtibwa Sugar imepania kupata vipaji vipya ambavyo vitajumuishwa katika kikosi chake. |
Tayari imeanza kufanya
kazi hiyo jijini Dar es Salaam kupitia kwa benchi lake la ufundi.
Kocha wake Mkuu, Mecky
Maxime na msaidizi wake, Zuberi Katwila ndiyo wamekuwa wakiendesha zoezi hilo.
Siku chache zilizopita,
zoezi hilo lilifanyika kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
“Lengo ni kuchagua
vijana kadhaa wenye vipaji ambao tunaamini watakuwa msaada baada ya kukaa na
sisi.
“Lakini pia tunaangalia
nini cha kuongeza katika kikosi chetu kulingana na mahitaji yetu,” alisema
Maxime.
Mtibwa Sugar ni kati ya
timu chache ambazo huwainua wachezaji wasiokuwa na majina, au huwapa nafasi
wachezaji wanaoonekana wakongwe na wameisha hadi wanapoibuka na kuwa lulu tena.







0 COMMENTS:
Post a Comment