Kiungo wa Simba, Jonas Mkude, hali yake
ni tete baada ya kupata maumivu ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja tangu
Jumamosi iliyopita.
Mkude yuko pamoja na kikosi cha Simba
visiwani hapa wakijiwinda vikali kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara
lakini yeye tangu Jumamosi amekuwa hafanyi mazoezi magumu kutokana na maumivu
hayo.
SALEHJEMBE lilishuhudia Mkude akiwa nje ya uwanja wakati timu hiyo ikifanya mazoezi
magumu na aliingia dimbani kufanya mazoezi mepesi tu.
Imeelezwa kuwa ugumu wa mazoezi ya
viungo yanayoongozwa na kocha wa viungo wa timu hiyo, Dusan Momcilovic, ndiyo
yanayochangia wachezaji wengi kuumia.
“Kweli mazoezi ni magumu mno, kila siku
tunalala hoi,” alisema mchezaji mmoja wa timu hiyo ambaye hakutaka kutajwa
jina.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe,
ameliambia gazeti hili kuwa maendeleo ya Mkude ni mazuri na atarejea uwanjani
hivi karibuni.
“Siwezi kusema atarejea lini lakini ni
hivi karibuni ndiyo atakuwa fiti kabisa,” alisema Gembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment