Kocha
wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kilifanya vema na
kufa makosa kadhaa katika mechi dhidi ya Uganda kuwania kucheza michuano ya
Chan.
Lakini
akasisitiza kuna mabadiliko makubwa ambayo yamejionyesha na yanaweza kuwa
msaada baadaye katika kikosi hicho.
Stars
ilitoka sare ya bao 1-1 na wenyeji wake Uganda katika mechi iliyopigwa kwenye
Uwanja wa Nakivubo, Kampala.
“Utaona
kulikuwa na mabadiliko makubwa na tunaweza kuendelea kufanya mabadiliko zaidi
kwa kuwa tumekuwa na muda mfupi sana.
“Matumaini
yetu kama benchi la ufundi kubadilika zaidi kwa ajili ya mechi zijazo,” alisema
Mkwasa.
Kwa
sare hiyo, maana yake Stars imetolewa kwa jumla ya mabao 4-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment