July 22, 2021

 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa anahofia kula chakula akiwa mbele ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kutokana na kile anachodai ni chuki kali aliyonayo kiongozi huyo.


Kupitia sauti ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao sauti ya mtu anayesadikika kuwa ni Manara imesikika ikisema kwamba miongoni mwa vitu ambavyo vinampa shida ndani ya Simba ni roho ya chuki.



"Barbra wewe una chuki na roho mbaya sijawahi kuona mpaka naogopa kula chakula mbele yako. Umekuwa ukiwadhalilisha wafanyakazi wa Simba jambo ambalo ni baya," ilisikika sauti hiyo.


Pia habari zinaeleza kuwa Manara anampango wa kubwaga manyanga Simba mara baada ya fainali Kigoma Julai 25 ambapo itakuwa ni Yanga v Simba, Uwanja wa Lake Tanganyika,  Kombe la Shirikisho.

33 COMMENTS:

  1. Sijui na huku Mzee Mpili atakuwa anahusika au??

    ReplyDelete
    Replies
    1. MANARA hana adabu. Kwanza kabisa anamdhalilisha mwanamke kwenye mitandao mchana kweupe hii sio nzuri.Hawa ni mama zetu dada zetu ukiachana na masula ya kimajukumu tunapaswa Kama wanaume kudili nao kwa heshima na ukiachana kuwa Barbara ni mwanamke mkuu wako wa kazi ni mkuu wako wa kazi huwezi kwenda kumtukana kwenye mitandao ya kijamii. Na Manara hawezi kuwa mkubwa kuliko bosi wake wa kazi na hapo ndipo tatizo linapoanza. MANARA anafikiri untouchable ndani ya Simba. CEO wa taasisi sio mtu wa kudhalilishwa na msemaji wa klabu hii sio haki hapa MANARA lazima awajibishwe asifikiri akiondoka Simba ndio mwisho wa Simba.Kama Manara kachukizwa na vitendo vya Barbara basi taratibu zipo za kuwasilisha malalamiko yake kistaarabu lakini sio kwenda kumtukana mkuu wako wa kazi mitandaoni hii haikubaliki hata kidogo,mpira sio Kazi ya wahuni. Kwa hili sio Barbara anaeivuruga Simba Kama Manara anavyotaka kuwaaminisha wanasimba na Umma wa watanzania na Dunia ni dhahiri shahiri Manara ndie mwenye matatizo. Hasa ukichukulia yakwamba Manara kaanzisha zengwe hili siku chache kabla ya mechi ya fainali ya FA.Hizo hoja za Barbra anazozilalamikia Manara kuwa anamtuhumu kuihujumu Simba zitakuwa zinamshiko kutokana na timing ya Manara kuachia malalamiko yake kipindi hiki Cha ukaribu wa mechi ya fainali.Kama walikuwa na ugomvi ni mambo ya ndani ya klabu na Kazi vipi leo Manara aamue kuchafua hali ya hewa ndani ya klabu kipindi hiki Cha maandalizi ya mechi muhimu? Hivyo Kuna mtu alishamsikia Barbara akidemka hovyo kulumbana na mtu yoyote mitandaoni au public kuhusiana na kazi? Inaonekana kabisa kuwa Barbara yupo very proffesional na Manara ni Kama mtu aliokotwa mitaani very unprofessional. Wanasimba Manara asituchukulie kuwa ni mizezeta atatuburuza vyovyote anavyotaka yeye. Kweli anafanya kazi nzuri ya kuhamisha ila anapokosea hasa kuhatarisha usalama na utulivu wa klabu lazima aambiwe hadharani kuwa amekosea na kutokumchekea hata kidogo hata kama anatishia kuondoka Simba basina aondoke kwa amani lakini alichokifanya Manara kwa Barbara na Simba sio sawa hata kidogo na inasikitisha.

      Delete
    2. Manara kazoea kuwanyanyasa wanawake kwa kisingizio kuwa yeye anaonewa. Mwanaume gani wa hovyo anaejiliza kwenye mitandao kama mdada aliachwa na mpenziwe?

      Delete
  2. Hizo ni tetesi na njama za kuwatoa kwenye umoja. Siku hizi kuna watu wanajaribu kutengeneza vitu. Haji Manara kwa ninavyomfahamu si mtu wa kuogopa kitu na kukimbilia kuongea wazi kiasi hicho. Simba ina uongozi wenye kufuata mambo yake kiutawala. Sijaamini

    ReplyDelete
  3. Umeshawahi kufanya kazi na ponjoro wewe au unawaona tu ukipishana nao?
    Hawapendi na hawataki kuona mtu mwingine awe juu na kupewa attention zaidi yao hasa kama akiwa hana mchango wa hela

    ReplyDelete
  4. Hujielewi itabidi ufanyiwe checking

    ReplyDelete
  5. Waongo hakuna kitu chochote kwa manara mbona ypo frxh tu na anauwamin xan uwongoz wake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa aina ya uandishi wako unaonesha ni wa aina ya kizazi cha awamu ipi.Akili za kizazi chenu ni ngumu kuelewa

      Delete
  6. Amesema kweli, hamfutilii mambo mnabisha tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndo unaebisha maana unapingana na kauli halisi ya mhusika.
      Huenda hujamsikiliza Manara ukapata kuelewa

      Delete
  7. Naomba tu MUNGU mfungwe mechi ya j2, hapo kuna jitu litakufa au kuachia ngazi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Manara alishasema, tukifungwa trna Kigoma anaachia ngazi. Hapa anatuandaa kisaikolojia tu. Tukishinda watatuambia wameyamaliza viongozi. Tukifungwa Manara atasema naachia ngazi kwa sababu nahujumiwa nk

      Delete
  8. Manara hana nidham, anatakuwa kuadhibiwa kama kweli ni sauti yake. Huwezi kutoa povu la kiounbavu kama hilo

    ReplyDelete
  9. Inawezekana kweli anawapa muchongo yanga

    ReplyDelete
  10. Manara WWE Ni mpambe acha kubishana na mke was boss utaludi ccm tena,Barbra Ni msomi WWE mlopokaji,ukiendelea na jeuri yko utalipwa 200000 badala ya 700000 ndo maana we kibarua uwez kuajiliwa coz busara empty

    ReplyDelete
  11. Tusidharauliane kwa sababu wewe ni tajiri mimi ni masikini au wewe umesoma mimi ni ngumbaru,hadhi na utu wa mtu uko pale pale bila kujali hali yake,elimu yake,nafasi yake,rangi yake,muonekano wake au sura yake n.k

    ReplyDelete
  12. SAA chache baada ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez kumjibu Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara baada ya kusambaa sauti mitandaoni, msemaji huyo ameibuka tena na kujibu juu ya sauti hizo.
    Manara amedai kuwa hakusambaza sauti hizo zilizokuwa gumzo mtandaoni akimtuhumu Barbara kumfanyia mtimanyongo ndani ya klabu hiyo, jambao ambalo Mtendaji huyo alisema hana muda wa kulijadili kwa sasa kwa vile akili zake zimeelekezwa katika fainali ya ASFC.
    Manara ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akidai hajasambaza sauti hiyo kama watu wanavyodhani na ataliongelea jambo hilo mechi yao dhidi ya Yanga Julai 25 mkoani Kigoma ikiisha.
    "Jana nilisema sitaongea tena kuhusu hili jambo hadi game ipite na mamia ya watu wamenirai hivyo pia. Lakini Kwa sababu anazozijua yeye usiku wa jana akaamua kuvujisha clip niliyomtumia yeye WhatsApp!!"
    Ameandika kuwa; "Wengine wanadhani mm ndio nimeituma hyo clip, sina muda na hivyo vitu, lau ningetaka kuachia lolote jana , basi ningeachia mambo ya aibu na tuhuma zake zilizojaa vitisho kwangu."
    Manara ambaye anafahamika kwa jina la utani Bugati amewataka mashabiki wa timu hiyo kuelekeza fikra zao kwenye mechi ya Jumapili kisha wamsubiri ataongea zaidi.
    "Narudia tena na tena sitaki kwa sasa kuongea lolote hadi mechi hii ipite, nisilazimishwe kusema sasa. Yoyote anaedhani vinginevyo asubiri Jumatatu kisha tutoe hukumu. Sitachafuka na ukweli utaniacha huru na mtajua kila kitu. Focus yetu tuipeleke Kigoma tafadhali, nikiyasema sasa Simba ndio itaumia," ameeleza Manara.

    ReplyDelete
  13. Mi nadhani hata sisi Yanga tusishabikie,zaidi tujipo geze kwa Mungu kutuonyesha ukweli wa upande wa Pili wa Hawa watu hususani Haji tumekuwa tukilalamika kauli zake leo tumeng,amua na Mungu ameonyesha madhaifu yake,Mimi nadhani Barbra Ni mkubwa kuliko Haji na amesajiliwa na Mo lkn Haji anaongea na Mamlaka kubwa saana

    ReplyDelete
  14. Haji hakutakiwa ku overreact tunaambiwa Club inaendeshwa kisasa hii Nini Sasa Simba Ina Management au haijaizinishwa (mabadiliko bado)?maana hii kali .Na Tatizo hapa Ni mtu kujichukulia madaraka mkononi ,Mimi huwa nashangaa nakujiuliza mipaka ya msemaji wa Timu Ni ipi? Na je kila asemalo huwa linatoka kwenye Utawala?So kwa hili tukio Kama Ni la kweli nimempata jibu na darasa kwa kweli.

    ReplyDelete
  15. Breaking News: Mpya kama walivo dedturi yao Yanga hawamtaki Ahned Arajiga kuwa refa wa mechi ya tarehe 25. Woga ndio ugonjwa wao. Wanataka refa mwengine. Jee watasilizwa wachague wamtakae sheria zuvunjwe

    ReplyDelete
  16. Ndio hatumtaki specifically huyo, apewe mwingine yeyote

    ReplyDelete
  17. Huyo refa ndiye aliwahadaa Wachezaji wa Azam,akatoa faulo ambayo Ni Kona then akaruhusu Goli la kihuni,mechi ya KAGERA na Simba Goli la kusawazisha la Simba Offside na kwanini yeye tu mechi za Simba?wewe godoro toka raundi ya Kagera Refa yeye,hiyo katusaidia Haji

    ReplyDelete
  18. Salehe Kadata hata umbea umemshinda eti wapo wanasuruhisha,kumbe mnamlipa laki Saba tuuuuuuu

    ReplyDelete
  19. Manara, GSM yupo nawe usiingie mkataba wa 4 mil na simba. Yanga itaendelea kukulipa na kukutunza. Wewe zidisha uweledi katika mipango tulokubaliana. Tunataka yanga iwr juu kwa hali yoyote

    ReplyDelete
  20. Manara Yuko sahihi coz wanawake wa siku hizi ni wajinga mna wakiwa na madaraka wanajiona wao ni Kama mungu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hivyo mama yako ni mjinga pia?

      Delete
  21. Bila ya mama ungemjua Mungu?

    ReplyDelete
  22. Mwanaume uwe na kifua ona babra hajaongea Wala kureply chochote huyo msomi anajielewa shida elimu ya haji manara basi Kama amekosa elimu angezunguka kuona watu wanaishije kuliko kutukana

    ReplyDelete
  23. Yaani hiyo taaarifa inakufanya usipost habari nyingine kweli Simba na Mujahidina lao moja,toka Jana mmesinyaha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic