July 27, 2021

 

KAMA ulikuwa unadhani Klabu ya Yanga inatania katika kesi yao dhidi ya Bernard Morrison basi jua kuwa klabu hiyo ipo siriazi na hiyo ni baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa michezo CAS kuweka wazi kuwa utaisikiliza kesi hiyo Alhamisi ya Julai 29,2021.


Hapo awali CAS 
walitoa taarifa kuwa wangeisikiliza kesi hiyo Julai 23 ambapo baadaye walitoa taarifa kuwa siku ya Eid Al Haji ilisababisha wao kusogeza mbele ambapo Jumamosi kupitia tovuti yao waliweka ratiba ya kesi watakazosikiliza ikiwepo ya ile ya Yanga na Bernard Morrison.

 

Kupitia tovuti hiyo ya CAS wameorodhesha kesi tatu zitakazosomwa hivi karibuni ambapo kesi namba CAS 2020/a/739 Yanga SC na Bernard Morrison, itasikilizwa Julai 29 huku kesi inayofuatia ikisikilizwa Agosti 5 yenye namba CAS 2021/a/7799 Yeni Malatyaspor na Mitchell Glenn.

 

Kwa upande wa uongozi wa Yanga, umesema kuwa bado unafuatilia kesi ya winga Bernard Morrison ambaye amehamia Simba, huku wakiweka wazi kuwa wanaamini haki itatendeka,huku wakiamini kuwa Simba watapokonywa ubingwa waliouchukuwa kwa kuwa wamemchezesha mchezaji asiyekuwa halali.

 

Bernard Morrison kwa sasa anacheza katika Klabu ya Simba, ambapo kabla ya kujiunga na klabu hiyo alikuwa akiichezea Yanga, huku usajili wa kuhamia Simba ukigubikwa na utata mkubwa wa kimkataba.

 


Aidha baada ya Morrison 
kujiunga na Simba, Yanga waliamua kupeleka kesi hiyo katika mahakama ya usuluhishi CAS ambayo mamlaka hiyo inaendelea kufanyia kazi kesi hiyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassani Bumbuli alisema kuwa watu wanatakiwa wawe watulivu kuhusu kesi hiyo kwani bado inafanyiwa kazi na mamlaka husika hivyo baada ya maamuzi watawapora Simba ubingwa wa ligi.

 

“Haki itatendeka juu ya kesi hii, watu wanaona kama ni utani kuhusu hii kesi ila ipo siku watafahamu kuwa kweli Yanga ilikuwa haitanii,hivyo mashabiki wa Yanga wanatakiwa kuwa wapole kwani hata ubingwa huu waliouchukua Simba tutaupora baada ya kesi kukamilika”, alisema kiongozi huyo.

26 COMMENTS:

  1. Subirini mpewe huo ubingwa, mbona kelele nyingi? Na mkipewa mtaufurahia kweli?

    ReplyDelete
  2. Kikubwa haki itendeke ili kuweka heshima kwa wahuni wengine wanaondoka bila utaratibu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umetamka vyema

      Delete
    2. Kweli kabisa na wahuni wanaolazimisha mikataba na kuchana sehemu za sahihi

      Delete
  3. Kesi ni ya Morrison na Yanga, Morrison aliruhusiwa na Chama cha soka cha nchi husika kucheza timu anayoitaka, akapewa Leseni na Chama Cha Soka cha nchi husika leo unahusishaje Ubingwa wa Simba na Morrison au Yanga? Kama kuna keshi ya Kimkataba ni juu ya Yanga na Morisson

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huo ndiyo ukweli mchungu wanaotakiwa viongozi wa Yanga kuwaeleza mashaniki ma wanachama wao. Mchezaji alipewa hadi leseni ya kufanya kazi Tanzania (ya kucheza mpira) na mamlaka husika baada ya TFF kumwombea kibali afanye kazi Simba. Sasa TFF ndiyo mamlaka iliyosimamia mchakato wote kihalali.

      Delete
    2. Tulia mbona unaogopa tusubiri majibu usiwe na mhaho

      Delete
    3. Hakuna cha Kutulia katika hili. Gloria na huyo jamaa wako sahihi kabisa! CAS haiwezi kuipa adhabu yoyote ile Simba kwa vile Morrison aliruhusiwa kicheza Simba na hata Yanga walipokata rufaa bado TFF waliruhusu acheze Simba. Kama Yanga wakishinda Sana sana Mchezaji atalipa fine na kurudishwa Yanga au kufungiwa kwa muda. Hakuna zaidi

      Delete
    4. Yanga bado wana ndoto za ubingwa kumbe 😅😅😅

      Delete
  4. Viongozi wa Yanga wanajifariji lakini wanajua kabisa kuwa hata kama wakishinda kesi hiyo hakuna namna yoyote ya kuweza kumvua ubingwa Simba. Waliwaahidi mambo mengi wanayanga na hakuna walilofanikiwa kwa hiyo wanaichukulia kesi ya Morrison kama ngao yao mbele ya mashabiki wao

    ReplyDelete
  5. Hahaha. Kesi inasoma yanga vs Morrison. Sijui ni ufahamu mdogo au ni mihemuko katika uandishi. Ubingwa said Simba unainguaje hapo Sasa🤗🤗🤗. Poleni Sana kwa kutamani yaliyo juu ya uwezo wenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani unaikumbuka vizuri kesi yenyewe ilivyokaa? Au ndo umeanza kuisikia leo?

      Delete
  6. Masikini utopolo mpaka wanatia huruma wivu wote huo njaa ya makombe,chezeni mpira sio judo kisha mbakimbilia kuomba ubingwa wa mezani,hamjitambui.

    ReplyDelete
  7. Ahhh ni kweli mnayosema. Hata tukipewa huo ubingwa sisi hatuna sifa hata moja ya kuitwa mabingwa. Nilipouangalia mpira wetu juzi kigoma sikuona iwezo wowote ila maguvu na faulo tu. Sasa tukiingia Caf champion itakuwa kipigo baada kipigo. Maana marefa huko hawana udugu wala urafiki wala hawapokei rushwa kama tulivyozowea. Hapo itakuwa fedheha kwetu na taifa. Chondd chonde viongozi yanga mtakuja kutupaka mavi

    ReplyDelete
  8. Kuna kitu mashabiki awakielewi juu ya kesi ya Morrison, endapo Morrison atashindwa kesi ni moja kwa moja itaiathiri na simba kwa maana mechi zote alizocheza simba itapokonywa pointi kwa kuwa walifaidika nae kwenye iyo michezo isivyo halali, hivyo suala la kwamba aliidhinishwa na tff halina nafasi kwa maana cas ndo combo cha juu na cha mwisho kwenye maamuzi na rufaa inaweza kutengua maamuz yoyote yale ysliyopitishwa ngaz ya chini ndo maana ya rufaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtangoja sana,unadhani viongozi wa Simba ni mambumbumbu mpaka wamchezeshe mechi zote kwa kutolijua hilo,watani nyie jipangeni vizuri kwa season ijayo tu huu ukurasa ndo ulishaisha kama ni movie unatakiwa usome"THE END"
      hahaha sinema za zamani,na wachezaji wenu wafundisheni kucheza mpira sio karate vinginevyo kimataifa mtaabisha.

      Delete
  9. Mikia mhalo wa nini tulizeni hapo.......unafikiri team zinazopokwa points huaga mchezaji hajaruhusiwa ety..... Tulizeni MACHUPI FC

    ReplyDelete
  10. Njia pekee ya kupata Ubingwa iliyobaki ni wa mezani vinginevyo hatutapata tutaambulia kuwa Wazee wa Viti Maalum CAF Champions League kila siku kubebwa. Hivyo lazima tutumie kila njia

    ReplyDelete
  11. NANI MWENYE MAMLAKA YA KUSAJILI WACHEZAJI, TFF, CAF ,FIFA ILIPITISHA VIPI KUCHEZA HAWAKUONA HILO TATIZO. SASA SIMBA INAHUSIKAJE NA MAAMUZI YA CAS WAKATI KESI NI UTO NA MORRISON????

    ReplyDelete
  12. MACHUPI FC mbona mmeingiwa na mhalo....tulizeni unyero dawa yenu inakuja

    ReplyDelete
  13. Kwa CAS wanaitambua Simba au kesi Yanga walilalamika Morrison kuvunja makubaliano ya kucheza bure wakati mkataba umekwisha. Nafikiri wakifanya mchezo Yanga watapigwa faini wao. Maana had mchezaji anaondoka hakuwa na mashahara wa miezi minne.

    ReplyDelete
  14. Utopolo acheni hivyo chezeni mpira








    mchukue ubingwa wahalali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic