Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amewashangaza mashabiki wa soka
visiwani hapa, baada ya kuacha kuwafanyisha mazoezi wachezaji wake na
kukimbilia jukwaani kuwaelewesha mashabiki.
Kikosi cha Simba juzi
kilifanya mazoezi yake kwenye Uwanja a Amaan lakini mashabiki wa timu hiyo
waliohudhuria walionekana kutofurahia mbinu ambazo kocha huyo alikuwa
akizitumia, wakaanza kumpigia kelele, ndipo alipoamua kupanda jukwaani na
kuzungumza nao kwa lengo la kuwaelewesha.
Kerr, raia wa Uingereza, aliwaeleza mashabiki wa timu hiyo kuwa
anatengeneza kikosi chenye washambuliaji wenye uwezo wa kupiga mashuti.
Programu ya mazoezi ya kocha huyo, ilikuwa ni kupanga
washambuliaji watano na mabeki wanne wanaocheza kwa kuchuana huku wengine
wakisubiri na wanapomaliza muda wao, wanaingia wengine.
Kwa upande wa mashabiki, walisema haijawahi kutokea kuona kitendo
hicho Zanzibar, kocha kutoka nje ya uwanja na kwenda kuwafahamisha mashabiki
jinsi anavyofundisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment