Pamoja na ugumu wa mashindano, straika mpya wa Yanga, Donald Ngoma, amesema atahakikisha anapigana kufa na kupona
ili aubakize Yanga ubingwa wa Kombe la Kagame.
Ngoma raia wa Zimbabwe aliyetokea katika timu ya
Platinum FC ya nchini humo, alianza kwa mkosi michuano hiyo kwa kupata kadi
nyekundu dhidi ya Gor Mahia ya Kenya na
kumlazimu kukosa mchezo mmoja, lakini aliporejea alifanya kweli na kufanikiwa
kuwa mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya KMKM, wiki iliyopita.
Ngoma raia wa Zimbabwe amesema ana kibarua kigumu kuhakikisha anajituma
ili kuonyesha kiwango na kuisaidia timu yake hiyo kutwaa ubingwa, kwani ndiyo
faraja yake.
“Nahitaji kujituma na kuonyesha kiwango katika michuano hii na
katika ligi ili kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa kwani nitafurahi sana kuona
timu yangu inashinda na kutwaa ubingwa.
“Kuhusu mchezaji wa kupangwa naye uwanjani ili niweze kufiti,
yeyote kati ya (Malimi) Busungu na (Amissi)
Tambwe nikipangwa naye nitafiti, kwani kinachotakiwa ni kuelewana uwanjani,”
alisema Ngoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment