Mshambuliaji
mpya wa Yanga, Donald Ngoma amelambwa kadi nyekundu.
Ngoma
amepigwa kadi hiyo baada ya kumsukuma beki wa Gor Mahia ambaye alipanda kwenye
mguu wake katika dakika ya 24 ya mchezo.
Mechi hiyo ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame inaendelea sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tukio
hilo lilionyesha kumuudhi Ngoma raia wa Zimbabwe aliyekuwa na kadi ya njano
tayari, akamsukuma na mwamuzi akampa kadi nyingine ya njano na kuwa nyekundu.
Ngoma
alijikuta akiangua kilio baada ya kutolewa nje . Hadi sasa Yanga ina bao moja
kama ilivyo kwa Gor Mahia ambayo ilisawazisha katika dakika ya 24 kupitia
Shakava.







0 COMMENTS:
Post a Comment