MIGI AKISAINI KUICHEZEA AZAM FC KWA MIAKA MIWILI, LEO. Kiungo Jean Baptiste Mugiraneza 'Migi' amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam FC. |
Mugiraneza raia wa Rwanda ameanguka saini leo
kuichezea Azam FC itakayoshiriki michuano ya Kombe la Caf.
Kiungo huyo tayari alianza mazoezi na Azam FC ikiwa ni
pamoja na kusafiri nayo hadi Tanga ilipocheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya
Coastal Union pia African Sports.
Pamoja na kusaini kuichezea Azam FC, Mugiraneza ataondoka
kurejea Rwanda, halafu atarejea nchini akiwa na timu yake ya APR ambayo
ataichezea katika michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es
Salaam kabla ya kujiunga rasmi na Azam FC baada ya michuano hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment