Hatimaye mshambuliaji wa Yanga, Mliberia, Kpah Sherman kutimkia zake
Afrika Kusini (Sauz) kuwa sawa na leo hii anatarajia kuondoka zake kwa ajili ya
kwenda kufanya vipimo vya Afya.
Uongozi wa Yanga, tayari umeshatoa baraka zake kwa mshambuliaji
huyo ambaye inadaiwa kuwa ameuzwa katika Klabu ya Mpumalanga Black Aces
inayoshiriki Ligi Kuu ya Sauz.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa, taratibu
zote za Sherman kujiunga na timu hiyo zimekamilika na kilichobakia ni vipimo
vya afya yake. Endapo atafuzu, basi msimu ujao hataonekana katika michuano ya
Ligi Kuu Bara.
“Sherman anaondoka kesho (leo) na kwenda Sauz kwa ajili ya vipimo
vya afya na endapo atafuzu basi hiyo ndiyo itakuwa tiketi yake ya kuiaga
Tanzania.
“Hata hivyo, kwa upande mwingine, sisi Yanga tutafaidika na
mamilioni ambayo tumemuuza huko na tunatarajia kuyatumia kusajili mchezaji
mwingine wa kimataifa ambaye atachukua nafasi yake,” kilisema chanzo hicho cha
habari ambacho hakikuwa tayari kutaja kiasi ambacho ameuzwa mchezaji huyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro, alipoulizwa
juu ya safari hiyo ya Sherman, hakuwa tayari kuizungumzia zaidi ya kudai: “Sijui
ataondoka lini lakini kama utaenda uwanjani leo (jana) usipomuona basi ujue
ameondoka na kama utamuona jua kuwa ataenda siku yoyote kuanzia kesho (leo).”
Yanga imeamua kumuuza mchezaji huyo kutokana na kile ninachodaiwa
kuwa ni shinikizo kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm
ambaye anadaiwa kutomhitaji katika kikosi chake, japokuwa baadhi ya viongozi
walikuwa wakitaka abaki.
0 COMMENTS:
Post a Comment