OLUOCHI |
Simba bado inaendelea kumtupia jicho kipa wa Gor Mahia, Boniface
Oluoch.
Oluoch ni mmoja wa wachezaji wanaowaniwa na Simba.
Kipa huyo raia wa Kenya, hivi sasa yupo nchini akiwa na timu yake
ya Gor Mahia inayoshiriki michuano ya Kombe la Kagame iliyoanza hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe,
alisema kuwa uongozi bado unahitaji muda kwa ajili ya kuangalia uwezo wake akiwa
golini akiokoa michomo, hivyo wametoa muda wa kumuangalia kipa huyo.
Hans Poppe alisema, ni ngumu kumpima kipa na kumsajili kwenye
mechi mbili au tatu, hivyo wametoa muda zaidi kwa ajili ya kumuangalia kwenye
mechi zijazo za Kagame zinazoendelea.
Aliongeza kuwa, hawana hofu juu ya uwezo wake, lakini kikubwa
wanachotaka ni kujiridhisha kipa huyo ana uwezo wa kuidakia Simba na kumpa
upinzani Ivo Mapunda pekee.
“Ni ngumu kumsajili mchezaji kwa kumuangalia kwenye mechi mbili au
tatu pekee, kama uongozi tumetoa muda zaidi kwa ajili ya kuuangalia uwezo wa
kipa huyo kwenye mechi zijazo za Kagame.
“Kipa huyo amedaka mechi tatu pekee, ambazo kama uongozi tumetoa
muda zaidi wa kumuangalia,” alisema Hans Poppe.
Kipa huyo hadi hivi sasa amedaka mechi tatu dhidi ya Yanga,
Khatoum na KMKM zote amefungwa bao moja moja na kufanya aruhusu mabao matatu
pekee.
0 COMMENTS:
Post a Comment