July 1, 2015

ISIHAKA...
Ikiwa ni siku mbili tu tangu kufuzu vipimo vya afya kwa mshambuliaji mpya wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma, beki na nahodha wa Simba, Hassan Isihaka amejitapa kuwa, straika huyo hatafua dafu watakapokutana uwanjani, kwani hata Jaja alikuja kwa mbwembwe lakini akazimwa.


Ngoma ametua nchini Jumamosi iliyopita na juzi Jumatatu alifanyiwa ‘check up’ ya afya yake katika Hospitali ya Msasani Peninsula chini ya Dk Humera Gajiyani, ambapo amethibika kuwa fiti.

Isihaka amesema kuwa Simba hawatishiki na ujio wa mshambuliaji huyo, kwani hata alipotua Mbrazili, Geilson Santos ‘Jaja’, mashabiki waliongea sana lakini alizimwa uwanjani.

“Kila mtu anasema lake kuhusu huyo Ngoma, lakini uwezo wa mchezaji unaonekana uwanjani siyo kupitia midomo ya mashabiki. Hata alivyokuja Jaja maneno yalikuwa mengi mwisho wa siku kila mtu aliona kilichotokea.


“Kwa hiyo na yeye zipo timu atakazozitesa lakini siyo ukuta wa Simba,” alisema Isihaka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic