Simba
imetoa mafunzo ya soka kwa tiku ya Black Sailor kwa kuichapa kwa mabao 4-0.
Black
Sailor ambayo imepanda Ligi Kuu Zanzibar msimu huu ilikiona cha moto, kwani
hadi mapumziko Simba ilikuwa ba mabao mawili.
Abdi
Banda ndiye alianza kuifungia timu yake bao dakika ya nne tu baada ya kupokea
pasi nzuri ya Dani Alves au Hassan Kessy na Kadabra Ibrahim Ajib akaongeza la
pili katika dakika ya 23.
Simba
ilipata mabao yake mengine katika dakika dakika 80 na 90 wafungaji wakiwa ni Elius
Maguli na Boniface Maganga.
Wakati
wote, Kocha Dylan Kerr alikuwa akisisitiza timu hiyo kucheza kwa kushambulia
sana.
Hii
ni mechi ya pili ya kirafiki ya Simba mjini hapa, mechi ya kwanza ilishinda kwa
mabao 2-0, yaliyofungwa na mkongwe Mgosi na Hamis Kiiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment