Manchester
United imemsainisha kipa ‘mtaamu’ wa Argentina, Sergio Romero kwa mkataba wa
miaka mitatu.
Kipa
huyo mwenye miaka 28, anachukua nafasi ya mkongwe Victor Valdes aliyetibuana na
Kocha Luois van Gaal.
Romero
aliwahi kufanya kazi akiwa anafundishwa na van Gaal wakati wakiwa katika klabu
ya AZ Alkmaar mwaka 2009.
Kipa huyo mwenye uwezo wa juu maana yake
ataongeza ushindani na David De Gea ambaye imekuwa ikielezwa anataka kujiunga
na Real Madrid.
0 COMMENTS:
Post a Comment