Hatua ya Robo Fainali ya michuano
ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuanza
kesho Jumanne kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Mchezo wa kwanza utakua ni kati ya
Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR ya Rwanda itakayotoshuka
dimbani saa 7:45 mchana kucheza na vijana wa Kwesi Appiah timu ya Al Khartoum
kutoka nchini Sudan.
Saa 10:15 kamili jioni, Gor Mahia
mabingwa wara tano wa michuano ya Kagame watashuka dimbani kucheza na Malakia
kutoka Sudan Kusini, viingilio vya michezo hiyo ya jumanne cha chini kitakua ni
elfu tatu (3,000) na kiingilio cha juu kitakua ni elfu kumi na tano (15,000).
Robo fainali zitaendela siku ya
jumatano, ambapo michezo miwili itachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam huku macho na masikio ya wapenzi wa mpira Afrika Mashariki yakielekezwa
kwa mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
Kabla ya mechi hiyo ya wapinzani
wa soka nchini Tanzania kuchezwa majira ya saa 10 jioni, mchezo wa kwanza
utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy kutoka nchini Sudan.
Viingilio vya mchezo wa siku ya
jumatano, kiingilio cha chini ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilo cha juu
kitanua ni elfu ishirini (20,000).
Katika hatua hiyo ya robo fainali
endapo timu zitacheza kwa dakika 90 na mchezo kumalizika kwa sare, hatua
itakayofuata ni kumpata mshindi kwa matuta (penati).
IMETOLEWA NA BARAKA KIZUGUTO WA TFF.
0 COMMENTS:
Post a Comment