![]() |
| MUUAJI WA YANGA: OLUNGA, NI HATARI... |
Yanga
imepoteza kwa bao 2-1 katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Kagame.
Gor
Mahia, mabingwa wa Kenya ndiyo walioibuka na ushindi katika mchezo huo mtamu
uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika kipindi cha kwanza.
Lakini
Gor Mahia wakazidi kutamba katika kipindi cha pili kwa kupata bao la kwanza
kupitia kwa mshambuliaji wake Michael Olunga.
Olunga
aliyekuwa akiisumbua ngome ya Yanga tokea kipindi cha kwanza alifunga bao hilo
baada ya kuwatoka Kelvin Yondani na Mbuyu Twite.
Yanga
walitangulia kupata bao katika kipindi cha kwanza baada ya Gor Mahia kujifunga
baada ya krosi ya Donald Ngoma, hiyo ilikuwa dakika ya 5.
Dakika
ya 16, Shakava akasawazisha kwa kichwa baada ya Juma Abdul kumuangudha
Walusimbi.
Dakika
ya 24, Ngoma akalambwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje.
Nahodha
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alikuwa
na nafasi ya kusawazisha kwa Yanga baada ya kupiga mkwaju wa penalty, kipa
akaudaka.
Mwishoni
mwa kipindi cha pili Yanga walicharuka na kushambulia mfululizo lakini
haikuwazuia Gor kukomaa na kubakiza ushindi wao wa kwanza dhidi ya Yanga.








0 COMMENTS:
Post a Comment