July 26, 2015

TAMBWE BAADA YA KUFUNGA LEO....
Yanga imefikisha pointi 9 baada ya kuitwanga Al Khartoum ya Sudan kwa bao 1-0 katika mechi yake ya mwisho ya makundi katika Kombe la Kagame.

Shujaa wa Yanga alikuwa Amissi Tambwe aliyefunga bao lake katika kipindi cha kwanza lakini sasa kinachoangaliwa ni Yanga kukutana na Azam FC.

Yanga inakutana na Azam FC katika mechi ya robo fainali itakayopigwa Jumatano kwenye dimba hilohilo la Taifa.

Timu zote zimeshinda mechi tatu za hatua za makundi, lakini Yanga ilicheza mechi zaidi ambazo ni nne na kupoteza moja.

Kwa mechi hiyo, maana yake hatua ya nusu fainali Tanzania itakuwa imebakiza timu moja.


Kwa maana nyingine, Tanzania ina uhakika wa kuingiza timu katika nusu fainali ingawa moja itakayobaki itakuwa na kazi ngumu kuingia fainali na ikiwezekana kulibakiza kombe hilo linaloshikiliwa na APR.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic