MGETA (WA PILI KUSHOTO) AKIWA MAZOEZINI NA KIKOSI CHAKE CHA NECKARSULMER. |
Beki wa pembeni
wa zamani wa Simba, Emily Mugeta ameendelea kupambana kuhakikisha anapata namba
katika kikosi cha kwanza katika timu yake ya Neckarsulmer
inayoshiriki daraja la tano
nchini Ujerumani.
Mugeta amesema
mazoezi yamekuwa makali, lakini anajifunza mambo mengi na zaidi anapambana
kupata namba.
“Napambana
kumuonyesha kocha ninaweza, ninaonyesha juhudi na kufuata maelekezo. Lengo
langu ni kupata namba.
“Mpira wa huku
una ushindani mkubwa sana, kwangu mambo kadhaa ni mageni lakini najifunza huku
nikitafuta nafasi,” alisema Mgeta.
Mgeta amewahi
pia kukipiga katika kikosi cha Polisi Morogoro kabla ya kutua nchini Ujerumani.
0 COMMENTS:
Post a Comment