Beki wa kulia wa Yanga, raia wa Ghana, Joseph Zuttah, ameanza
kuyaona maisha yake katika klabu hiyo kuwa magumu baada ya kudai kuwa ana kazi
kubwa ya kufanya ili kuhakikisha anapata nafasi ya kudumu katika kikosi cha
kwanza cha timu hiyo.
Zuttah amejiunga na Yanga hivi karibuni akitokea Klabu ya Medeama
ya Ghana na kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo ambayo kwa
sasa inajiandaa na Michuano ya Kagame inayoanza kutimua vumbi Jumamosi hii hapa
nchini.
“Kusema kweli bado sina
uhakika wa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza ila anayejua hilo ni kocha.
“Nasema hivyo kwa sababu nafasi ninazocheza uwanjani zote zina
wachezaji mahiri na wenye uwezo mkubwa, kwa mfano Juma Abdul, Salum Telela,
Mbuyu Twitte na Simon Msuva, wote ni wazuri, hivyo kocha ndiye anayejua kama
nastahili kuwepo katika kikosi chake cha kwanza,” alisema Zuttah.








0 COMMENTS:
Post a Comment