August 1, 2015



Beki wa kati na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amekubali kushindwa katika Kombe la Kagame baada ya kutolewa katika robo fainali, lakini amewataka mashabiki wasubiri kuona kivumbi chao katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.


Yanga iliyotolewa katika robo fainali na Azam FC kwa kufungwa penalti 5-3, inatarajiwa kuweka kambi jijini Mbeya kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa ligi kuu Septemba 12, mwaka huu.

Cannavaro alisema kilichotokea katika mchezo wao na Azam ni bahati mbaya tu, hivyo mashabiki watulize mawazo, wasubiri kuna vitu vyao kwenye ligi.

“Kwa sasa nguvu zetu tunazielekeza katika maandalizi ya ligi ili tuweze kuwa na kiwango kizuri na ninaamini tutaleta ushindani kutokana na viwango vya wachezaji.


“Kinachotakiwa hivi sasa ni kila mchezaji kusahau kile kilichotokea na hata mashabiki watuvumilie kwa yaliyotokea ila wasubiri kuona kivumbi chetu kwenye ligi,” alisema Cannavaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic