Gwiji wa zamani wa, Thierry Henry ameshindwa kuficha
mapenzi yake kwa kikosi hicho baada ya kumshauri Kocha Arsene Wenger ahakikishe
ananunua mshambuliaji.
Henry ameyasema hayo wakati akichambua mechi kati ya
Arsenal dhidi ya Liverpool ambayo iliisha kwa sare ya bila mabao.
Kwa sasa Henry ni mchambuzi wa runinga maarufu ya
michezo ya Sky ya Uingereza.
Alisema anaamini kwa washambuliaji waliopo Arsenal,
bado hawana uwezo ambao anaamini wataisaidia Arsenal.
Alisisitiza Arsenal ina wachezaji wengi wazuri lakini
wanaonekana kuwa na asili ya viungo.











0 COMMENTS:
Post a Comment