Hawa ndiyo mabingwa
wapya wa Kombe la Kagame.
Wanaitwa Azam FC.
Azam FC iumeifunga Gor
Mahia kwa mabao 2-0 na kubeba ubingwa wa Kagame wakiwa hawajafungwa hata bao
moja.
Mwaka 2002, Tusker ya
Kenya ilifanya hivyo, lakini Azam FC imefanya hivyo huku ikiwa haijafungwa hata
bao moja, Simba na Yanga hazijawahi kufanya hivyo.
Bao la kwanza la Azam
FC lilifungwa na John Bocco ambaye aliipangua beki ya Gor kabla ya kupiga krosi
safi kabisa iliyomfikia Bocco akamaliza kazi.
Bao la pili, likafungwa
Kipre ambaye alipiga mpira wa adhabu na kipa wa Gor akadhani unatoka.
Baada ya hapo, Gor
iliendelea kupambana lakini ilishindwa kuukamata mziki wa Azam FC ambao
walikuwa safi huku beki Serge Wawa akimtuliza mshambuliaji hatari Michael
Olunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment