KIKOSI CHA FREE STATES BILA NGASSA... |
Wakongwe Kaizer
Chiefs wameifunga Free State Stars kwa mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu
Afrika Kusini (PSL) katika mechi iliyopigwa jijini Johannesburg.
Chiefs
wameishinda Free State anayoichezea Mtanzania Mrisho Ngassa ambaye hata hivyo
dakika zote 90 alikuwa kwenye benchi.
Ngassa aliendelea
kubaki kwenye benchi huku Kocha Kinah Phiri akifanya mabadiliko yote matatu
bila ya kumteua.
Bao safi la
Siphiwe Thshabalala lakini mawili mawili ya kujiunga ndiyo yalichangia kuiua
Free State.
Kutokana na
kipigo hicho, timu ya Ngassa sasa inashika mkia katika PSL baada ya kucheza
mechi mbili na kupoteza zote
WALIOKUWA BENCHI:
Diakite, Makhaula,
Angula, Somaeb, Thethani, Ngasa, Fileccia
0 COMMENTS:
Post a Comment