Mwanariadha maarufu wa Uingereza, Mo Farah mwenye asili ya Somalia
ameshinda mbio za ubingwa wa IAAF zinazofanyika jijini Beijing, China huku akiwaacha
wanariadha wa Kenya ambao walionekana watakuwa tatizo kwake.
Farah ameshinda mbio ndefu za mita 10000 akiwaacha Wakenya watatu ambao
walikuwa wamemzunguka ikionekana walikuwa wakifanya juhudi mmoja wao aibuke na
ushindi.
Hata hivyo, Farah alionekana kuwa fundi zaidi yao kwa kuwazidi ujanja na
kuibuka mshindi katika hatua za mwisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment