Kiungo Mkenya, Victor Wanyama amesema anataka kuondoka katika kikosi cha
Southampton.
Wanyama ameuambia uongozi wa Southampton inayoshiriki Ligi Kuu England
kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo.
Sababu ya msingi aliyoitoa ni kwamba hana raha klabu hapo, angependa kutafuta au kuendeleza maisha yake ya soka sehemu nyingine.
Habari hiyo imeonyesha kuushitua uongozi wa klabu hiyo ambayo
inamtegemea kama kiungo namba moja mkabaji.
Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwa Wanyama hadi kufikia baadhi ya timu
ikiwemo Manchester United kumuweka kwenye listi ya wachezaji inayowawania.
0 COMMENTS:
Post a Comment