Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15),
kimerejea leo asubuhi kutokea kisiwani Zanzibar kilipokwenda kucheza michezo ya
kujipima nguvu na kombani ya U-15 ya kisiwani humo.
Katika michezo miwili iliyocheza kisiwani humo, iliweza kushinda michezo
yote miwili, (4-0 ), (1-0), huku kocha Bakari Shime akiwapongeza vijana wake na
kusema wanaendelea kuimarika kuelekea kujiandaa na kuwania kufuzu kwa
fianali za Mataifa Afrika chini ya miaka 17 mwakani.
Baada ya kurejea jijini Dar es salaam leo, kambi ya timu hiyo imevunjwa na
vijana hao watakutana tena mwisho wa mwezi wa Agosti kama ilivyo katika program
yao ya kukutana kila mwisho wa mwezi na kucheza michezo ya kirafiki.
Mwishoni mwa mwezi Agosti timu hiyo ya vijana inatarajiwa kuelekea mkoani
Tanga kucheza michezo ya kirafiki na kombani ya mkoani humo, ambapo kocha wake
Shime pia anatumia nafasi hiyo kutazama wachezaji wengine wenye uwezo mzuri
katika timu za kombaini za mikoa kwa ajli ya kuwaongeza katika kikosi chake.
Mpaka sasa timu hiyo ya vijana chini ya miaka 15 (U15) imeshafanya ziara na
kucheza michezo katika miji ya Mbeya na kisiwani Zanzibar.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment